Kiongozi wa kidini nchini Pakistani anatoa mafunzo ya fikra
za Osama bin Laden kwenye shule za dini kwa Wanafunzi takriban 5,000.ingawa
serikali ya nchi hiyo inapambana na wanamgambo wa Taliban kaskazini magharibi
mwa Pakistani, haina mipango ya kuzifungia shule zinazotoa elimu kwa watoto
kuunga mkono wanamgambo wa Taliban.
Imamu wa msikiti mmoja mjini Islamabad Abdul Aziz Ghazi
amesema wana malengo sawa na Taliban lakini amesema hawatoi mafunzo ya kijeshi.
Kiongozi huyo amesema wanatoa mafunzo kuhusu misingi ya
Jihad ila ni juu ya wanafunzi kupata mafunzo ya kijeshi baada ya kutoka shuleni
hapo.
Ghazi anamiliki shule nane za kidini yaani Madrasa,moja ya
shule yake iliwahi kufanya ziara ya kwenda kukutana na Osama Bin Laden nchini
Afghanistan.
Hivi sasa wasichana 3,000 na wavulana 2,000 wanasoma kwenye
taasisi zake.
Mitaala ya shule zake inatoa mafunzo ya kusoma Quran,
kiarabu na thiolojia,hesabu na sanaa inaonekana kuwa masomo ya kidunia, vitabu
vingi vimeandikwa na Ghazi na kuchapishwa katika shule hizo zenye vyumba vya
kuchapisha.
Katika moja ya shule, kuna maktaba iliyopewa heshima ya jina
la bin Laden .
No comments:
Post a Comment