Maafisa wa polisi wanachunguza kisa kimoja ambapo wezi
walivunja na kuingia katika nyumba ya mchezaji wa kilabu ya Southampton Victor
Mugubi Wanyama nchini Uingereza na kumuibia mali yake usiku wa jumatatu.
Shati moja la kiungo wa kati wa timu ya Barcelona Andres
Iniesta ,pamoja na nguo za wanamitindo kadhaa pamoja na jozi 20 za viatu ni
miongoni ya vitu vilivyoibwa.
Wezi hao pia waliiba gari la mchezaji huyo aina ya Land
Rover lenye thamani ya shilingi millioni 8.4 fedha za kenya,fanicha,Runinga
pamoja na vifaa vyengine vya kielektroniki .
Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 23 anaishi katika nyumba
ndogo na polisi wameshangazwa kwamba majirani zake hawakuamshwa na kelele za
uvunjaji huo.
Kikosi cha timu yake ya Southamptom kilikuwa kimesafiri hadi
Villa ambapo bao la dakika za mwisho liliifanya mechi hiyo kuwa na sare ya 1-1.
Wanyama ameshiriki katika mechi 14 msimu huu na kufunga
mabao matatu huku Southampton ikiendelea kupigania nafasi ya kufuzu katika
mechi za UEFA.
Ni mchezaji aliyeuzwa kwa kitata cha juu kutoka Uskochi
baada ya Celtic kumuuza kwa pauni 12.5 mnamo mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment