Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Job Ndugai
Leo ikiwa ni tarehe 5 Novemba, 2014, Kwenye Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania (JMT), Kikao cha pili, mkutano wa 16 / 17.
- Kikao cha bunge leo kimeongozwa na Naibu Spika wa Bunge,
Mhe. Job Ndugai.
- Hati za kuwasilisha mezani ni kutoka Wizara ya fedha,
Ofisi ya Rais, na Kambi ya Upinzani.
- Naibu Waziri wa fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba alianza kwa
kuwasilisha hati za Wizara ya fedha mezani.
- Waziri wa nchi, ofisi ya Rais Sera na uratibu, Stevene
Wassira amewasilisha pia hati ya mpango wa maendeleo.
- Kambi ya Upinzani, nayo imewasilisha hati yake.
Kipindi cha maswali
na majibu:
Swali la kwanza linaelekezwa katika Wizara ya nchi, Ofisi ya
serikali, Uhusiano na Uratibu.. Swali linahusu masuala ya uwekezaji. Majibu
yanatolewa kwa ufupi na kueleweka.
Swali la pili sasa linaelekezwa kwa ofisi ya Waziri mkuu,
TAMISEMI, Kuhusu ni vipi serikali imejipanga katika ujenzi wa barabara kwa
kiwango cha lami mpaka kufikia mwaka 2015. Swali hili limeulizwa kwa niaba ya
Mbunge wa Arumeru.
Swali linalofuata ni kwa Wizara ya fedha, ambalo linaulizwa
na Mbunge Agustino Lyatonga Mrema, Kuhusu kwanini mishahara ya watumishi wa
serikali inachelewa wakati tayari Wizara imeshatengewa bajeti? Swali linajibiwa
na Naibu spika wa Bunge, Mhe. Mwigulu Nchemba, anatoa ufafanuzi.
Mbunge wa Rombo, Mhe. Selasini anauliza swali la nyongeza
kuhusu ni hatua zipi zitachukuliwa kwa watumishi walioshiriki katika kupitisha
malipo ya mishahara hewa?
Mwigulu anajibu na kusema hatua ya kwanza ni kusimamisha
malipo hayo, na la pili ni kuwawajibisha watumishi hao ikiwa itabainika
ilifanywa kwa makusudi. Anaendelea kutoa Ufafanuzi.
Mbunge wa viti maalum wa singida, Diana Chilolo, anauliza
swali la nyongeza: Kwanini fedha zilizokombolewa zisitumike kulipa madeni ya
walimu?
Mhe.Mwigulu anasema umeandaliwa mfumo maalum wa malipo ambao
utaepusha mlolongo wa malimbikizo ya madeni ya Walimu pamoja na watumishi
wengine wa serikali ili kuepusha usumbufu.
Sasa ni Maswali kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa:
Swali la kwanza limeulizwa kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya
Somalia na Kenya kuhusu kudai Kisiwa cha Pemba, Mhe. Bernard Membe anajibu kuwa
hajapokea taarifa rasmi kutoka katika serikali hizo, ila amewataka Watanzania
kuondoa hofu kuhusu hilo kwani Kisiwa cha Pemba ni mali ya Tanzania.
Swali kutoka kwa Mb. Khalifa Khalifa, anauliza kuhusu wavuvi
wavamizi wanaokuja kuvua ndani ya mipaka ya Tanzania, je serikali imejipanga
kukabiliana nao vipi ili kuepusha mgogoro na uhusiano mbaya na nchi wanazotoka
wavuvi hao?
Mhe. Membe anajibu kuwa serikali italishughulikia hilo.
Swali lingine linaulizwa kuhusu kesi za kimataifa katika
mahakama ya ICC, Nini mtazamo wa nchi za Afrika kuhusu kushitakiwa kwa viongozi
wakuu wa nchi?
Anajibu kuwa nchi za Afrika zimesikitishwa na hilo kwani
inajenga taswira kuwa nchi za afrika hazina uwezo wa kushughulikia masuala
yake, jambo ambalo limetafsiriwa kuwa ni aina nyingine ya changamoto ya Afrika
na nchi za Magharibi kama ilivyokuwa ubaguzi wa rangi na kadhalika.
Na amesema Kutokana na hilo, zipo baadhi ya nchi za Afrika
zimetishia kujitoa katika uanachama wa ICC.
Na Katika kujibu swali la nyongeza kuhusu ni vipi serikali
ya Tanzania itaepuka kushitakiwa kwenye mahakama hiyo,
Mhe. Membe amejibu kamwe serikali ya Tanzania haiwezi kushitakiwa
kwa kuwa viongozi wake wanafanya kazi nzuri.
Ni zamu ya maswali kwa Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo
ya makazi:
Kwa niaba ya Waziri, Mhe. Simbachawene anatoa majibu, ambapo
swali liliulizwa ni lini mgogoro baina ya wakulima na wafugaji utafikia kikomo?
Jibu: Wizara imetambua kwamba ugomvi unasababishwa na uhaba
wa ardhi kulingana na mahitaji na ongezeko la watu na mifugo, ndio kimekuwa
chanzo kikuu cha mgogoro huo, Hivyo basi Wizara itahakikisha serikali inaanza
utaratibu wa Kupima ardhi na kutoa mpango wa matumizi bora ya ardhi. Anaendelea
kutoa maelezo...
Maswali kwa wizara hii bado yanaendelea..........
Wizara ya Kazi Na Ajira:
Swali linaulizwa kuhusu Ukosefu wa Ajira kwa vijana
wanaomaliza elimu ya juu, Je serikali inawasaidia vipi vijana kupata mikopo ili
waweze kujiajiri? Na kwanini vyeti vyao visitumike kama dhamana ya kupatia
Mikopo kwa kuwa hawana cha kuweka rehani katika taasisi zinazokopesha?
Mhe Gaudencia Kabaka, Anatoa ufafanuzi kuwa bado serikali
haijafikiria kutunga sera hiyo, na anaeleza kuwa kazi ya serikali ni kuandaa
mazingira ya wananchi wake kupata huduma kwa urahisi.
Swali la nyongeza, Mb. Viti Maalum anauliza: Je, kwanini
elimu ya ujasiriamali isipewe kipaumbele ili angalau vijana na wananchi waweze
kupata uwezo wa kuanzisha hata biashara zisizo rasmi ili kupunguza tatizo la
Ajira?
Mhe Waziri anajibu kuwa ni wazo zuri na anasema ni jambo
ambalo zipo taasisi za elimu kama VETA linatoa ujuzi mbalimbali ambazo
zinawawezesha vijana kuweza kuzitumia kujiajiri.
Swali lingine ni kutoka kwa Mhe. Msabaha, anahoji kwanini
serikali isiweze kuvitambua vipaji na kuviendeleza ili viweze kuwakwamua vijana
kujiajiri?
Jibu linatolewa kuwa, Serikali inavitambua vipaji na ipo
kwenye mchakato wa kuviwezesha ili vitoe ajira kwa VIjana ambao wataweza
kuajiri na wengine.
Sasa ni Wizara ya Maliasili na Utalii:
Kuhusu vipuri vilivyokamatwa, je ni hasara kiasi gani
serikali imepata na imejipanga vipi kuzuia tatizo la ujangiri lisiendelee?
Jibu kwa niaba ya Waziri: Hasara za kiuchumi ni takribani,
Bilion 3, 4, 680 000, Na mpk sasa serikali imewakamata majangiri 556 na kesi
zao zinaendelea, na bado Wizara inachukua hatua mbalimbali za kupambana na
Ujangiri, kama vile kuhifadhi na kuimarisha ulinzi, kutoa mafunzo zaidi kwa
watumishi na kuwapatia vifaa vya kutosha vya kutendea kazi.
Swali la nyongeza: Je, Wizara imejipanga vipi kushughulikia
hizo kesi za Majangiri ili Wananchi waweze kuridhika na hatua watakazochukuliwa
hawa waporaji wa mali za umma?
Anajibu: Kesi zitashughulikiwa haraka iwezekanavyo.
Mhe. Anna kilango Malecela anauliza swali la nyongeza: Kama
Serikali inapambana na Ujangiri, kwanini inatoa vibali vya Uwindaji?
JIbu: Hili ni suala la kimkataba, kwahiyo kama lina haja ya
kujadiliwa, basi serikali itabidi ilitazame upya.
Swali: Sekta ya utalii ni moja ya chanzo kikubwa na cha kasi
cha mapato, Je serikali imejipanga vipi kudhibiti swala la athari za utamaduni?
Jibu: Kukua na kuingiliana kwa utandawazi kunapelekea
mwingiliano wa watu na jamii tofauti, hivyo swala la kuathiriwa kwa tamaduni ni
changamoto kubwa, hata hivyo serikali imeweka mikataba itakayowawezesha wageni
kuheshimu mila na tamaduni za nchi. Na pia kuna mpango wa serikali wa kuweza
kuzuia matumizi ya teknolojia kulingana na umri. Pia Kuhusu mavazi, serikali
itatia mkazo suala la vazi la taifa.
Swali la Nyongeza, linahusu mavazi yasiyo ya kistaarabu
pamoja na tabia ambazo zipo kinyume na tamaduni, Je serikali inashughulikia
vipi tabia hizi zinazoshamiri kwa kasi katika jamiii?
JIbu: Malezi ni wajibu wa serikali na wazazi, kwahivyo kila
upande uwajibike ipasavyo.
Wizara ya Nishati na Madini:
Swali likiulizwa na Mb. Freeman Mbowe, kuhusu mpango wa
serikali kusambaza umeme vijijini, Hususani kwa Wilaya ya HAI mkoani
Kilimanjaro.
Naibu Waziri Charles Kitwana anajibu kuwa serikali kupitia
wizara ya nishati inatarajia kuanza kusambaza umeme vijijini kupitia mradi wa
REA, na utekelezaji umefikia 26%.
Mhe. Joseph Selasini anauliza swali la nyongeza: Miundombinu
ya umeme Wilaya ya Hai imechakaa sana kiasi cha kupelekea madhara kwa wananchi
hadi vifo, Je serikali itachukua hatua gani ili kutatua uchakavu wa
miundombinu?
Jibu: Ni kweli, kutokana na baadhi ya miundo mbinu kuwa ni
ya muda mrefu ndio maana inachakaa, ila serikali kupitia Tanesco itaanza
mchakato wa kupitisha njia mpya za umeme kuanzia Dar es salaam hadi Segera,
kisha nyingine kuanzia Tanga na kuendelea huko vijijini kote. Mpango huo upo na
utafanywa haraka.
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika:
Swali: Kuna haja ya wakulima kuendelea kuzalisha mazao
ambayo hawana manufaa nayo baada ya kusainishwa vocha ambazo zilijaa
udanganyifu?
Jibu: Serikali inasikitishwa na udanganyifu ambao umefanyika
kwa wakulima kwa hizo vocha ambazo zimewanyima fursa ya kupata hata pembejeo
bora kwa ajili ya uzalishaji. Na nia ya serikali ilikua ni nzuri katika hili
jambo. Hata hivyo, serikali inawashikilia baadhi ya mawakala na itawachukulia
hatua kali za kisheria. Pia Wameisababishia hasara kubwa serikali.
Nyongeza: Kwanini serikali isitoe ruzuku moja kwa moja kwa
wakulima?
Jibu: Serikali itafanya mpango wa namna ruzuku zitakavyoweza
kuwafikia wakulima kupitia utaratibu maalum utakaoanzishwa. Kwa sasa Serikali
Imeanza na utaratibu wa kutoa ruzuku kupitia taasisi za fedha kwa mfano CRDB,
NMB na benki nyinginezo zimeanza kutoa huduma hiyo.
Muda wa Maswali na Majibu Umeisha...
==============================
============================== ===============
UPDATE:
Kikao cha Bunge kimehairishwa mpaka saa kumi Jioni na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Job Ndugai.
No comments:
Post a Comment