Mmoja
wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo
mfupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na
ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya
kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake
nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla.
Globu ya Jamii inaitakia kheri na fanaka Clouds FM katika kusherehekea miaka 15 tangu kuzaliwa kwake.
Ndafu wa shughuli akiwa mezani
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na
mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na
pale zikiwa zimetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
Msanii
mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha
ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15
tangu kuanzishwa kwake nchini.
Mkuu
wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya
Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa
kipindi cha XXL,Dj Fetty.
Dj
Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo
ya kutimizwa miaka 15 ya kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na
kwingineko.
Mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa
kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka
15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
No comments:
Post a Comment