Pages

Sunday, December 7, 2014

COMRADE MWIGULU NCHEMBA AUTEKA MJI WA GEITA


Mwigulu Nchemba akiwasili Uwanja wa MKutano Geita mjini.


Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba yakiendelea kwa shamrashamra za kutosha.

Hisia za Wananchi kwa Mwigulu Nchemba ambaye katika Bango moja wapo anasomeka kama SOKOINE WA PILI NCHINI TANZANIA.

Sehemu ndogo tu ya Maelfu ya Wananchi waliofika Kumsikiliza mh:Mwigulu Nchemba.

Kueleka 2015 haikukosa,Hizi ni hisia za Wananchi wanaokoshwa na Uchapakazi wa Mwigulu Nchemba

Mwigulu akikaribishwa Geita kwa Mabango.




Kiongozi wa ACT Kanda ya Ziwa(Mratibu) akitoa shukrani zake za dhati kwa Mwigulu Nchemba kwa namna alivyokuwa mfano kwa kutetea Masikini na Wanyonge ndani ya BUnge na Nje ya Bunge.

Mkuu wa Mkoa wa Geita akisalimia wananchi (Mwanamama)

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Msukuma akizungumza na Wananchi wake kuhusu Kero mbalimbali zinazowakumba ndani ya Mkoa wa Geita,Kubwa likiwa Wazawa kutopewa kipaumbele kwenye Madini,Pia unyanyasaji kwa Wachimbaji wadogo.

Comrade Mwigulu Nchemba wakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita wakati wa Mkutano hii leo.

Comrade Mwigulu Nchemba mbaye ni Naibu katibu Mkuu CCM Bara akionesha Ishara ya Dole "Mambo Poa" wakati akiwasalimia wananchi wa geita hii leo.


Tanzania Oyeeeeee,Hiyo ndio salamu ya Mwigulu Nchemba mara zote apandapo Jukwaani kuzungumza na Wananchi.

"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hatujazi nafasi,Tunatafuta viongozi wenye uwezo wa kusimamia Halmashauri zetu za Vijiji, Mitaa na Vitongoji ili ziweze kufanya kazi za Maendeleo kwa Uadilifu na Ufanisi wa hali ya Kuridhisha"

Hii ni sehemu tu ya Maelfu ya Wananchi wa Geita waliofika Kusikiliza Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mwigulu Nchemba,Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Kero za Wananchi wa Geita.

Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi kuchagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi kwasababu ndio wenye sera inayotekelezwa,Hivyo wanajua mahitaji ya Wananchi wao.


"Kuna Wananchi wanatamani sana kubadirisha Vyama kama Nguo,Kubadirisha vyama sio suluhisho la Kutatua kero za Maendeleo.Tujitahidi kufanya maamuzi yenye tija wakati wa uchaguzi,tuchague Viongozi imara na wenye nia ya kuwaongoza.Achaneni na kubadirisha vyama vya siasa"

Kupanga ni Kuchagua

Naibu katibu Mkuu akisisitiza kuwa hakuna atakaye ichafua Tanzania yeye akabaki salama,Hakuna atakaye Iba mali ya Umma akatembea kifua mbele.Wahujumu Uchumi wote wa Nchi hii waanze kujiandaa kisaikolojia.

Muonekano wa Umati wa Wananchi waliotulia wakisikiliza hoja za Msingi kutoka kwa Mwigulu Nchemba.

Comrade Mwigulu Nchemba akisisitiza Jambo kwa Wananchi wa Geita Mjini kuhusu Uchaguzi wa serikali za Mitaa.

Sehemu ya Wananchi wakati wa Mkutano huo.

Comrade Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Geita Mjini.

MKutano Umeshamalizika na Wananchi wanarejea makwao.

Awali Mkutano huu ulipaswa Kurushwa Live na Star Tv,Bahati mbaya Mitambo yao ilikwama kuurusha Mkutano.Tunaomba radhi kwa Usumbufu wowote uliojitokeza. 
Picha na Sanga Festo wa Habari Kwanza

No comments:

Post a Comment