Pages

Sunday, December 7, 2014

Kanusho Kutoka Ofisi ya Mbunge na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa Kuhusu Uvumi Uliozagaa Kwenye Mitandao Mbalimbali ya Kijamii Kuwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa Kulazwa nchini Ujerumani



 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa

Msemaji wa Waziri Mkuu Mstaafu  Mhe. Edward Lowassa,  
Bw. Aboubakary Liongo
----
 Ofisi ya mbunge na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, jana ilikanusha vikali uvumi uliozagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa mbunge huyo wa Monduli amelazwa nchini Ujerumani.

Taarifa zilizoenea zinaeleza kuwa Lowassa, ambaye wakati wote wa Mkutano wa 15/16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano uliofanyika kwa wiki tatu, hakuwepo bungeni, amekuwa Ujerumani ambako amelazwa kwa matibabu.


Hata hivyo, jana msemaji wake, Aboubakary Liongo aliliambia gazeti hili kuwa taarifa hizo ni za uzushi lakini akaeleza ni kweli yuko nchini humo kwa ajili uangalizi wa afya yake. 
“Aliondoka kwenda India kumuona (mbunge wa Kilindi) Beatrice Shelukindo ambaye amelazwa huko na baada ya hapo alimpeleka mke wake Ujerumani kwa ajili ya kutibiwa matatizo ya miguu,”
“Alipofika huko na yeye akaamua kuangalia afya yake kwa kuwa daktari wake yuko nchini humo.” alisema Liongo.
Alisema Lowassa atarejea nchini wiki ijayo kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za sikuku ya Uhuru itakayofanyika Desemba 9 na baadaye ataelekea Monduli kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 14.“Atakwenda kuhakikisha chama kinashinda nafasi zote katika uchaguzi huo,” alisema Liongo.

No comments:

Post a Comment