Nchini Tanzania kuna
maeneo machache ambayo baadhi ya watu wake hawana uelewa thabit wa kutumia mipira
ya kiume(Condoms) kiasi ambacho mpira mmoja unaweza kutumiwa na vijana watatu
hadi wanne kwa kubadilishana baada ya kuusafisha na kuanika juani.
Hali hiyo imeelezwa
kuwa chanzo kingine cha kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa
Ukimwi.
Mwandishi wa BBC Baruan
Muhuza alitembelea wilaya ya Longido kaskazini mwa Tanzania kijijini Orglay na
kuzungumza na mmoja kati ya vijana wa kijijini hicho.
No comments:
Post a Comment