Pages

Thursday, December 25, 2014

HAYA NDIO MANENO ALIYOYASEMA MAMA TIBAIJUKA BAADA YA RAIS KUTENGUA UTEUZI WAKE

Wananchi mkoani kagera wamepinga  uamuzi   wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete  kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba na makazi   na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakiongea  na ITV wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua  nini hatima ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk. kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine  waliohusika katika sakata hilo   na kumuuondoa waziri  Tibaijuka na pia wamebaki na sintofahamu ambapo wamemtaka  Rais  kutoa ufafanuzi kuwa licha kumg’oa madarakani kiongozi huyo  Je, Pesa  hizo zitarudishwa kwenye akauti hiyo  ya TEGETA ESCROW au la.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo katibu  wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi  mkoa wa Kagera Hamimu Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa  jana wakati  akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam  kwa kumuondoa kiongozi huyo huku katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo chadema  katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka  Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa za Escrow zitarudishwa  lini katika akanti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho  la kwamba pesa hizo hazirudishi?.


Kwa upande wake  aliyekuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi Profesa Anna Tibaijuka amesema  licha Rais kumuondoa katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa amerudi jimboni kwake kwaajili ya  kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi  ya  kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba Pesa hizo alipewa na lugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama  pesa hizo zilitoka katika akaunti ya TEGETA SCROW ndomaana hakutaka kujiuzuru mapema.

CHANZO: ITV TANZANIA

No comments:

Post a Comment