Eneo la tukio St Louis
maandamano makubwa yametokea nchini Marekani katika mji wa
St Louis yaliyosababishwa na askari kumpiga risasi kijana mweusi akiwa katika
kituo cha mafuta .Polisi wanamtetea afisa mwenzao ya kwamba alitenda kitendo
hicho kama njia ya kujihami ,baada ya marehemu kumnyoonyeshea bunduki katika
kitongoji cha Berkeley.
Waandamanaji waliyaanza maandamano hayo mara tu baada ya
taarifa za mauaji hayo
kusambaa,kutokana na hasira waliyonayo waandamanaji hao
picha za video zinawaonesha baadhi yao wakivuka mpaka waliowekewa na polisi .
kitongoji cha Berkeley kiko umbali wa kilomita tatu kutoka
mjini Ferguson, Missouri, mahali ambako yalifanyika mauaji ya kijana mwingine
mweusi aliyekuwa na umri wa miaka kumi na nane Michael Brown , aliyepigwa
risasi na askari wa kizungu,mauaji yaliyoibua hisia za ubaguzi wa rangi ,mauaji
ambayo yalitokea mwezi August mwaka huu .hata hivyo Brown hakuwa na silaha
yoyote wakati akiauwa.
No comments:
Post a Comment