Pages

Friday, December 5, 2014

HIVI NI VIKWAZO VITANO(50) WANAVYOKUTANA NAVYO WANAOPEWA UBOSI KWA MARA YA KWANZA

Hii haishangazi sana kuona watu ambao wanapata cheo kwa mara ya kwanza kukutana na vikwazo vya hapa na pale. Utafiti uliofanya na watu fulani umebaini kuwa kinachotokea ni kwamba wengi au karibu asilimia 50 ya mabosi wapya kabisa hawajawahi kufanyiwa mafunzo ya kupata nafasi hizo kama mameneja. Na hapa soma uone vyanzo vya vikwazo vyao vinatokana na ni nini?


1. Wengi hufikiri kwamba watakuwa na mamlaka makubwa zaidi
Inawezekana wengi wanapopewa nafasi hizo kwa mara ya kwanza wanafikiri wataongezewa uwezo wa mamlaka pale wanapoongezewa hayo majukumu. Makampuni huangalia watu wenye uwezo, utendaji mzuri na wenye mwelekeo ndio hupewa nafasi za umeneja, hivyo hufikiri wakifika juu watafanya maumuzi yao binafsi kuhusu mambo fulani. Kinachowashangaza wakifika huko juu, wanabanwa na kazi zaidi na hayo majukumu mapya waliyopewa kuliko walivyofikiri.
Wanajikuta kuna vitu vingi vinavyohitajika kutoka kwao ili wavitolee ripoti au maamuzi kutoka kwa wanaowaoongoza hadi kwenda kwa mabosi we wa juu zaidi. Hivyo huanza kukinzana na mambo ya majukumu ya kila siku. Kijana mmoja kutoka Harvard aliandika makala yake akasema “Kuwa meneja si kitu cha kufikiri utakuwa bosi bali unakuwa mateka.”

2. Wengine Hufikiri wanajua kila kitu

Kosa jingine mameneja wapya wanachofanya ni kufikiri wanajua kila kitu. Kama walizoea kuulizwa maswali na kutoa majibu mazuri na huenda na mtizamo huo huo kuwa we ni majibu ya kila kitu. Kama sehemu ya wafanyakazi wenzako kila mtu wazo lake ni la msingi wa kusaidia shirika au kampuni.





3. Wengi hushindwa kuelewa tofauti ya kusimamia na kuongoza
kila meneja mpya anatakiwa kujua kwa umakini na ufasaha tofauti ya kusimamia na kuongoza. Uzuri wa kila tofauti hiyo ni nana ambavyo unaweza kuwaachia watu wengine waweze kufanya kazi, meneja yeyote ni msimamizi wa kazi fulani kuhakikisha inafanyika kama inavyotakiwa. Kiongozi ni yule mtu anayeangalia na kuona mbali au kuonyesha mwelekeo wa shirika hilo na akaweza kugawanya majukumu kwa watu husk kulingana na uwezo na ujuzi walionao. Kiongozi anajua kufundisha watu anaowaongoza. Meneja yeye bado ana jukumu kwa timu kuhakikisha inafanikiwa au kushindwa, yeye ndiye anaruhusu wafanyakazi wengine wahusike hivyo nafasi yake iendelee kubaki kuliko kuipoteza.

4. Hazisaidii timu wanazoziongoza

Meneja mpya anatakiwa kujua kuwa timu zao ndio sura zao, hivyo wanatakiwa kuonyesha mfano ulio bora zaidi. Wanao uwezo wa kuonyesha mgawanyo wa kazi kwa kila mfanyakazi aliye chini yake na tabia ya timu yake inamfuata hadi kwenye nafasi yake. Meneja hupata sifa kutakana na timu anayoongoza na vile vile anatakiwa kuwajibika kwa timu nzima endapo haifanyi vizuri. Meneja anatakiwa kuwajulisha wafanyakazi wake kwamba wako pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa kusaidiana na kuelekezana kufikia mafanikio katika kitengo chao.

5. Wengine Hujaribu kuwa tofauti ni uhalisia wao wenyewe

Unahitaji kujua ujasiri wako na upungufu wako na ujue malengo yako wewe kama meneja mpya kwenye hicho kitengo. Hakikisha kuwa timu yako wanajua mipango uliyokuja nayo, malengo , mahitaji na mategemeo yako kwa kila mmoja na timu yako kwa ujumla. Vile vile hakikisha mawasiliano yako yanakuwa wazi ili kila mtu kwenye kitengo chako awe anakufikia kirahisi, mapema zaidi wakikutambua na wewe kuwatambua utapata matokeo bora zaidi na kwenye timu pia.

No comments:

Post a Comment