Ndege ya jeshi la muungano unaoongozwa na marekani.
Wapiganaji wa Islamic State nchini Syria wamedai kuidungua
ndege ya kivita ya muungano wa jeshi unaoongozwa na Marekani.
Shirika linalochunguza maswala ya haki za kibinadamu lenye
makao yake mjini London ambalo linaunga mkono upinzani nchini Syria limesema
kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na mji wa kazkazini wa Raqqa unaodhibitiwa na
IS.
Shirika hilo linasema kuwa rubani, raia mwarabu aliyekuwa
akiendesha ndege hiyo ametekwa.
Baadhi ya ripoti zinadai kuwa rubani huyo ni raia wa
Jordan.Jordan ni miongoni mwa mataifa ya kiarabu ambayo yanashiriki katika
mashambulzi dhidi ya Islamic State.chanzo bbc
No comments:
Post a Comment