Joseph Nkaissery ndio waziri mpya wa usalama nchini kenya
Waziri mpya wa usalama nchini Kenya, Joseph Nkaissery leo
ameapishwa rasmi na kuanza kutekeleza wajibu wake kama waziri akikutoa onyo
kali kwa maafisa wa usalama kwamba ni lazima wawajibike la sivyo watimuliwe.
Jenerali huyo mstaafu anasema raia wa Kenya wana haki ya
kupata usalama bora zaidi kutoka kwa maafisa wa polisi.
Nkaissery anamrithi Joseph Ole Lenku aliyetimuliwa kazini na
rais Uhuru Kenyatta mwezi uliopita. Emmanuel Igunza anaarifu.
Katika hotuba yake ya kwanza punde tu baada ya kuapishwa,
Nkaissery amesema anafahamu kuhusu mtazamamo wa umma wa kutokuwa na imani na
idara ya polisi nchini.
Lakini amesema anataka kukabiliana na hili kwa dharura kwa
kuwahimiza maafisa wote kuwawajibikia wananchi.
Vilevile ameitetea sheria mpya ya usalama iliyoidhinishwa
hivi maajuzi nchini ambayo imezusha mjadala mkali. Nkaissery amesema anaamini
kwamba sheria hiyo ya kukabiliana na ugaidi ambayo upinzani unaiona kuwa kali
inayokiuka uhuru wa wananchi itasaidia zaidi katika kukabiliana na tishio la
kundi la wanamgambo wa kiislamu kutoka Somalia, Al Shabaab.
Rais Uhuru Kenyatta amemteua Nkaissery baada ya msururu wa
mauaji yaliotekelezwa huko kaskazini mashariki mwa Kenya ambayo kundi hilo la
Alshabaab linatuhumiwa kutekeleza. Kundi hilo limetekeleza mashambulio kadhaa
ya kigaidi nchini.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment