Pages

Thursday, December 4, 2014

KITUMBO AMTAKA JAMHURI KIHWELO AMUOMBE RADHI SIKU SABA

Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akizungumza na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo amempa siku saba kocha wa timu ya Mwadui  Jamhuri  Kihwelo  amuomba radhi kwa kile alichodai kuwa ametoa lawama zisizo za kweli dhidi yake kupitia vyombo vya habari.

Akizungumza na waandishi wa habari Kitumbo alisema amesikitishwa na taarifa alizozitoa kocha huyo dhidi yake zinazomhusisha kuwa amekuwa akileta vurugu katika michuano ya ligi daraja la kwanza kwa madai kwamba amekuwa akifanya fitina kupitia kuwahonga  fedha  waamuzi ili timu mbili za mkoa wa Tabora Rhino Rangers na Polisi Tabora ziweze kufanikiwa kuingia ligi kuu Tanzania bara msimu ujao.


Kitumbo kupitia vyombo vya habari amemtaka kocha huyo Jamhuri Kihwelo kuthibitisha madai yake vinginevyo atamchukulia hatua zinazostahili kwa kile alichodai kuwa kiongozi huyo wa timu ya Mwadui amesema uongo.

Alisema kitendo cha kocha huyo kuelezea tuhuma dhidi yake kupitia Star Tv katika kipindi TUONGEE ASUBUHI ambazo alidai kuwa zimemharibia mwenendo wa kazi zake si za kweli na kuwataka watanzania kutomwamini kocha huyo ambaye si mkweli.

"Naomba kocha Jamhuri Kihwelo aniombe radhi kwa muda wa siku saba na ninampa siku saba kuanzia leo tarehe 3 Desemba 2014 na kama asipofanya hivyo asinilaumu kwa hatua nitakazozichukua,najua kuwa TFF wananisikia kwa haya ninayoyasema nitamfikisha kwenye vyombo vyenye mamlaka ya soka viweze kumshughulikia"alisema Kitumbo.

No comments:

Post a Comment