Pages

Thursday, December 4, 2014

Misiba ya vijana Matei na Ogunda yatikisa mji wa Dodoma

 Baadhi ya mahakimu,wanasheria na mawakili waliojitokeza kushiriki kuagwa kwa marehemu Joshua na Matei
 Baadhi ya mahakimu,wanasheria na mawakili waliojitokeza kushiriki kuagwa kwa marehemu Joshua na Matei


Wakili wa kujitegemea Mhe. Anthony Mavunde ambaye alihitimu siku moja na marehemu Joshua.
Majeneza yenye miili ya marehemu Joshua na Matei wakati wa ibada Uwanja wa Nyerere Dodoma.
 Mamia ya waombolezaji waliofurika katika Uwanja wa Nyerere mjini Dodoma kuaga miili ya marehemu Matei John Mmassy(mfanyabiashara) na marehemu Joseph Joshua Oguda Wakili wa kujitegemea na Mkufunzi katika Chuo Kikuu Cha St John wakiwa katika harakati za kutoa heshima za mwisho kwa miili nya marehemu.
Na Deusdedit Moshi
Misiba ya vijana wawili, Marehemu Matei John Mmassy, Mfanyabiashara na mmiliki wa Klabu maarufu mjini hapa ya Matei Lounge na Wakili wa kujitegemea na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha St.John, Marehemu Joseph Joshua Oguda waliofariki kwa ajali ya gari maeneo ya Ranchi ya mifugo, Narco iliyopo Kongwa mapema wiki hii wakitokea Mjini Morogoro vimetikisa mji wa Dodoma na Viunga vyake. 



Miili ya marehemu hao imeagwa leo kuanzia mchana katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika Uwanja wa Nyerere mjiji Dodoma.Marehemu watasafirishwa jioni hii.Matei atasafirishwa kuelekea maziko Moshi Mkoani Kilimanjaro na Joshua atasafirishwa kuelekea Musoma.

No comments:

Post a Comment