Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 1, 2014

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inauza Habari za ofisi ya Rais Kikwete?

Waingereza wanasema, the one who speaks the truth is loved by God!
 Rais wa nchi au Taifa lililojengwa katika misingi ya kidemokrasia ndani ya presidential system huwa anaajiriwa na wananchi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi ndani ya mkataba uliokubaliwa kikatiba katika nchi au taifa.
 Ndani ya presidential system, ofisi ya Rais huwa niya juu kabisa katika nchi au Taifa lolote hapa duniani.
 Habari za Rais kuhusu kile anachokifanya kila dakika kwa faida ya nchi au taifa ni lazima zipatikane bure na ziwafikie wananchi wake katika wakati unaolingana na hali halisi ya mawasiliano katika nchi au taifa.


Tanzania kwa sasa tumepiga hatua mbele katika Nyanja mbali mbali za mawasiliano kama internet, instant messaging, Internet forums, and social networking kama inavyobainishwa kwenye The Global Information Technology Report 2014 iliyotolewa kwenye World Economic Forum 2014. Tanzania kwa sasa tuko kwenye nafasi ya 125 kati ya nchi 148 ambazo zimefanyiwa research.

Kwa nchi za Afrika, Tanzania tuko kwenye nafasi ya 19 kama inavyobainishwa - HAPA

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kutambua umuhimu wa wananchi wake kupata habari ili kuwasaidia kukielewa kile anachokifanya kila dakika katika msingi wa uwazi na ukweli, ndiyo maana amelazimika kuunda kitengo cha mawasiliano na pia tovuti ya rasmi ya Ikulu achilia mbali tovuti ya Serikali na taasisi zake ili zifanye kazi ya kuwahabarisha wananchi wake chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.

Wafanyakazi wa Kitengo cha mawasiliano cha Rais wanalipwa kwa kutumia kodi ya wananchi na kwa maana hii, kuuza habari au kukasimisha habari za Rais kwa watu au kikundi katika mlengo wa kuziuza ni makosa katika utaratibu, kimaadili na kisheria.

Kumekuwepo na mchezo mchafu unaoendelea kwa muda mrefu katika kitengo cha Kurugenzi ya Mawasilino Ikulu. Huu mchezo mchafu unapaswa kulaaniwa na wananchi wazalendo kwa nguvu zote.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais wa Jamhuri wa Muungano imekuwa ikitumia habari za Rais kwa ajili ya kuwapatia maslahi zaidi baadhi ya watu/watumishi wa kitengo cha Mawasiliano ya Rais kwa kutumia mlango wa nyuma kinyume na taratibu au maadili ya kazi zao.

Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais Kikwete imekuwa ikitoa habari na kuzikasimisha(commission) kimaslahi kwenye blog ya mwananchi mmoja anayeitwa Muhidin Issa Michuzi mwenye blog inayoitwa Issamichuzi Blogspot badala ya kuzitoa moja kwa moja kwa wananchi kupitia tovuti ya Ikulu, Blog ya Ikulu au Idara ya Habari (MAELEZO) katika muda mwafaka.

Katika kunufaika zaidi na habari za ofisi ya Rais, Blog ya Muhidin Issa Michuzi imeweka kizuio, kwa kiingereza wanasema, block visitors from right clicking or disable "copy and paste" to protect blog source code ili kuhakikisha habari za Rais Kikwete haziwezi kuchukuliwa na media au blog nyingine baada ya kuziweka kwenye blog yake.

Kuiacha kwa maksudi/malengo Tovuti Rasmi ya Ikulu iwe outdated kwa mlengo wa kukasimisha habari wakati kuna watu wanalipwa kwa kazi hiyo ni ufisadi na wizi wa pesa za walipa kodi wa nchi.

Kutoa habari na Presidential Press release na kumpa kwanza Muhidin Issa Michuzi ili aziweke kwenye blog yake ili wananchi watembelee kwanza blog yake kwa manufaa ya kumpatia Issamichuzi Blogspot kipato kupitia wadhamini wa matangazo ndani ya blog yake ni uvunjifu wa taratibu na maadili ya utumishi achilia mbali sheria mama ya nchi kama ilivyoainishwa katika Sura ya Kwanza, kifungu cha 18(2) kinachohusu Haki ya Uhuru wa Mawazo kama kinavyosema, 18 (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Kwa sasa ukitembelea Tovuti Rasmi ya Ikulu, kwenye section inayoitwa kituo cha Habari. Habari inayoonekana ni mpya ni habari ya Jumanne, Oktoba 14, 2014, inayohusu Rais kutoa Hati za Uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 162 ambao walikuwa wakimbizi kutoka Burundi. Hii ni habari ambayo kwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tokea tukio litokee lakini ukienda kwenye Blog ya Muhidin Issa Michuzi unakutana na latest news kuhusu Rais Kikwete.


Ukitembelea kwenye sehemu ya Matukio katika Tovuti ya Ikulu unakutana na matukio ya Tuesday 4th March 2014 ambayo yanahusu Rais Kikwete alipotembelea vikosi vya JWTZ vya Komando Morogoro. Kwa sasa ni zaidi ya miezi minane tokea matukio, lakini kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Ikulu, hii ndiyo LATEST NEWS, lakini ukitembelea Blog ya Muhidin Issa Michuzi utakutana na matukio mapya kuhusu Rais Kikwete anavyofanya SOMA ZAIDI HAPA

No comments:

Post a Comment