Hasara inayotokana na mauaji yanayofanywa na makundi ya
wapiganaji wa kiisilamu ni vifo vya watu wasio na hatia
Uchunguzi wa BBC umebainisha kwamba mashambulio ya kijihadi
yanayofanywa na wapiganaji wa kiisilamu yalisababisha vifo vya zaidi ya watu
5,000 kote duniani mwezi Novemba.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, mauaji yaliyotekelezwa na kundi
la kigaidi la Al Qaeda yanaongezeko kwa ukubwa, kutokana na kuimarika kwa
mtandao huo ulioenea katika zaidi ya nchi 14 duniani.
Huku idadi kubwa ya wafuasi wa Al Qaeda wakiwa nchini Iraq,
Nigeria, Afghanistan na Syria.
Nchi nne zilizoathirika zaidi kutokana na mauaji
yaliyofanywa nawanaopigana jihadi, ni Iraq, Nigeria, Afghanistan na Syria,
ikiathirika kwa kiwango kikubvwa zaidi na asilimia 80 ya vifo vyote.
Mashambulizi yaliyofanywa na makundi ya jihadi, yaliwalenga
waisilamu wa madhehebu ya Shia wale walio wachache pamoja na wasuni wengine
Uchunguzi wa BBC uliofanywa kwa usaidizi wa kituo cha
kimataifa cha masomo ya itikadi kali, ulinukuu mashambulizi 664 kufanywa katika
mataifa 14.
Uchunguzi huo unalenga kuonyedha idadi ya vifo vinavyotokana
na vita vya majihadi kila mwezi na pia kutoa maelezo kuhusu changamoto
inayotokana na vita hivyo.
Uchunguzi huo ulionyesha kwamba takriban watu saba
walifariki kila saa mwezi Novemba kutokana na vita hivyo, ambavyo vimechochewa
na al-Qaeda, na makundi mengine ya wapiganaji wenye kufuata itikadi kama za
Al-Qaeda.
Uchunguzi huo ulipokea taarifa ya vifo vya watu 22 kutokana
na vita hivyo huku watu 168 wakijeruhiwa vibaya.
Abu Khattab mwenye umri wa miaka 13 anapata mafunzo kujiunga
na kundi la IS
Kundi la wapiganaji la (IS) wanaoendeshea harakati zao
nchini Syria na Iraq, walisababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.
Shambulizi lililofanywa dhidi ya msikiti, mjini Kano, ndilo
lilikuwa shambulizi kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu mwezi
Novemba.
Kati ya watu 5,042 waliouawa, wengi wao walikuwa raia wasio
na hatia.
Wanajeshi 1,723 ni miongoni mwa waliouawa huku takriban
wapiganaji 1,000 pia wakiuawa katika mashambulizi.
Athari kwa maisha ya wananchi wengi wa mataifa yenye vita
vya Jihad
Kulingana na uchunguzi huo, Nigeria ndio nchi hatari zaidi
kutokana na harakati za Boko Haram wanaolaumiwa kwa mauaji ya watu wengi sana.
Afghanistan ilikuwa nchi ya tatu hatari zaidi kutokana na
harakati za wapiganaji waTaliban.
Ripoti hio ilifanywa na shirika la BBC, ICRS na shirika
lengine lisilo la kiserikali lenye makao yake mjini London.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment