Hii leo kulikuwa na taharuki katikati mwa mji wa Nairobi
baada ya Punda waliokuwa wamepakwa rangi kupatikana wakizurura mjini humo.
Walikuwa na maandiko katika mwili wao yakisema: 'Tumechoka'
Neno 'Tumechoka' ni kauli mbiu ambayo ilitumiwa na mashirika
ya kijamii kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya utovu wa usalama nchini kote.
Kwa kutumia Punda, kupitisha ujumbe wao, ni dhahiri kuwa ujumbe wao umefika kwa wengi.
Wanaharakati hao, wamewahi kutumia Nguruwe kuonyesha walivyo walafi na wafisadi wanasiasa wa Kenya.
Punda hao walikuwa 22 na walifikishwa kati kati ya mji kwa Lori. Dereva wa lori hilo alisema kuwa alilipwa na mtu flani kupeleka wanyama hao mjini.
Lori hilo lilipofikishwa mjini, mwanamume aliyekuwa amekodisha lori hilo aliamua kutoka kwenye Lori na wanyama hao.
Polisi wamesema wanachunguza kujua nani waliofanya kazi hio.
Wanyama hao walinuiwa kutuma ujumbe kwamba wakenya
wamechoshwa na hali mbaya ya usalama, alisema mwanaharakti mmoja aliyekuwa
kwenye Lori hilo.
''Tumechoshwa na uongozi mbaya, '' alisikika akisema
mwanaharakati mmoja huku akiwaskuma Punda hao kutoka kwa Lori.
Polisi wanasema wanawasaka wale waliohusika na kitendo
hicho.
No comments:
Post a Comment