Kijana
Said ambaye aliteseka na uvimbe mkubwa usoni sasa amepona baada ya
kufanyiwa upasuaji katika Hospital ya CCBRT iliyopo jijini Dar.
Stori: Imelda Mtema na Hamida HassanINGAWAJE Said (38), mkazi wa Bagamoyo kwa Mtoro, Pwani ambaye aliteseka na uvimbe mkubwa usoni kwa miaka 12 sasa amepona baada ya kufanyiwa upasuaji katika Hospital ya CCBRT iliyopo jijini Dar.
Akizungumza na waandishi wa habari hii, Ngawaje alisema kwa sasa ana amani moyoni na kuhisi raha ya dunia baada ya kuteseka kwa muda mrefu huku akiamini hawezi kupona tena.“Mimi siamini kama ule mzigo mzito uliokuwa umefunika usoni wangu haupo, nilikuwa nashindwa kulala kwa mawazo, sasa hivi niko sawa,” alisema.
Ngawaje alisema matunda hayo ameyapata baada ya gazeti hili la Machi 11, mwaka huu kutoa habari yake ukurasa wa 15 akielezea matatizo yake, watu mbalimbali walimchangia fedha kwa ajili ya matibabu.
Muonekano wa uvimbe aliokuwa nao kabla ya kufanyiwa upasuaji.
“Halafu akajitokeza mfadhili mmoja ambaye alitoa fedha zote za
kufanyiwa upasuaji ambapo upasuaji wa kwanza alifanyika Julai 15, mwaka
huu na wa pili Oktoba 30, mwaka huu.“Kwa sasa hata kuoa naweza maana huko nyuma hakuna mwanamke aliyekuwa akinipenda kutokana na tatizo nililokuwa nalo, nawashukuru sana watu wa Gazeti la Uwazi kwa kutoa habari yangu na watu kunisaidia, kwa kweli nimemuona Mungu,” alisema Ngawaje.
No comments:
Post a Comment