Mwalimu wa shule ya umma nchini Uingereza amepatikana na
hatia ya kuwalawiti watoto wanaorandaranda mitaani nchini Kenya.
Simon Harris alipatikana na hatia ya makosa saba, ikiwemo
kuwadhulumu kingono watoto hao katika mji wa Gilgil.
Alipatikana na hatia katika mahakama ya Birmingham kwa
makosa manne ya kumiliki picha chafu zinazoonyesha uchi wa waoto wadogo.
Hata hivyo mahakama haikumpata na hatia ya kitendo cha
kuwabaka watoto hao.
Haris alikuwa anakabiliwa na maskosa 23 ikiwemo madai 18 ya
kuwadhulumu watoto.
Unyama huo ulitendwa wakati Harris alipokuwa anaendesha
shirika la kijamii la kuwasaidia watu mapema mwaka wa 1990.
Wakati kesi yake ilipokua inaendelea, wendesha mashitaka
walisema kuwa aliwahadaa watoto hao wavulana kwenda nye nyumbani kwake
iliyojulikana kama "The Green House", kwa kuwapa chakula na kuwapa
hifadhi.
Kabla ya kesi hio kuanza, Harris alikiri makosa sita ya
kuwadhuru watoto hao waliokuwa kati ya umri wa miaka 13-14 alipokuwa bado
mwalimu wa chuo cha Davon.
Awali alikuwa anakabiliwa na makosa 22 kuhusiana na dhuluma
hizo alizozitenda nchini Kenya lakini jaji Philip Parker QC alisema kuwa makosa
manne dhidi ya mtuhumiwa yaliodnolewa wakati kesi hio ilipokuwa inasikilizwa.chanzo bbc
No comments:
Post a Comment