Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 11 aliiba maelfu ya dola
kutoka kwa nyanyake na kisha kukodi taxi kumpeleka eneo la mbali kukutana na
kijana mwenye umri wa miaka 16 ambaye walikuwa wakiongea naye tu kupitia
mtandao wa Internet.
Wawili hao hawajawahi kuonana hata siku moja.
Msichana huyo Alexis Waller yuko salama na bukheri wa afya
na hatakabiliwa na kesi yoyote baada ya kitendo chake ambacho kimewashangaza
wengi.
Maafisa wanasema Waller aliiba dola elfu kumi kutoka kwa
chumba cha nyanyake katika mji wa Bryant, jimbo la Arkansas.
Baada ya kitendo chake cha wizi, msichana huyo alikodisha
taxi na kumtaka dereva kumpeleka kwa kijana huyo katika jimbo la Florida.
"nilisema nitaka kwenda mjini Jacksonville,
Florida," Waller aliambia shirika la habari la KARK. "kijana huyo
aliniuliza kama nina pesa na nikamwambia ndio. ''
Gharama ya safari yake ilikuwa dola 1,300.
Jarida la Arkansas Democrat-Gazette linasema kuwa Waller
alikuwa tayari amesafiri umbali wa maili 500 kuelekea kwa kijana huyo lakini
polisi waliweza kuwasiliana na dereva wa taxi hio na kuwafuata.
Wazazi wake walisema Waller aliwakasirisha sana lakini ni
afunei kwao kwani mtoto wao aliweza kurejea nyumbani.
No comments:
Post a Comment