Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine waandamizi wa serikali.Katikati wapili kushoto anayeshuhudia ni Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gervas Mdemu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa miongozo ya kazi(Standing Orders) Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla ya kuapa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla wa kuapa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba mtoto Gracious Mathayo Ntebo mjukuu wa mkuu mpya wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla ya kumuapisha mkuu huyo wa mkoa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Freddy Maro).
No comments:
Post a Comment