Watu nchini Marekani wameelezea ghadhabu na hasira zao
kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa mtaalamu wa wanyamapori Paul
Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda ili ku chunguza maumbile ya ndani ya
Nyoka huyo.
Lengo la utafiti huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake
duniani, ilikuwa ni kuchunguza maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana
katika msitu wa Amazon.
Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha
utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao
kipindi kilichokuwa kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda
akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha joto
mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani ya tumbo la
Nyoka huyo.
Paul na vazi alilotumia kuingia ndani ya Nyoka kabla ya
kushindwa na kusalimu amri
Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya
Anaconda mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa
ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka huyo.
Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa
kichwa chake huku wenzake wakimtazama.
Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa
limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
"sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe
sikutaka kujiumiza. ''
Paul anapenda sana kujihusisha na maswala ya wanyama hasa
Nyoka
"nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi
Nyoka huyo kwa vyovyote vile.''
''Mimi mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia
jaribio vazi langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka
huyo. ''
Lakini baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya
tumbo la Nyoka na kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa
angeumizwa na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha
kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa
anaumizwa.
''Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe
hapa.'' alisema Paul.
Namna ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na
Nyoka huyo bado ni muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake
hilo kwa saa tatu.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment