Takriban watu 100 wakiwemo wanafunzi 80 wameuwawa na wengine
wengi kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia shule moja
inayosimamiwa na jeshi huko Peshawar kaskazini - magharibi mwa Pakistan.
Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana
kujeruhiwa japo idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi.
Maafisa mjini Peshawar wanasema kuwa wanaume watano ama sita
waliokuwa na silaha waliingia shuleni hapo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi
.
Wanafunzi mia tano na waalimu walikuwa katika shule hiyo ya
umma ya kijeshi wakati sham,bulizi hilo lilipotokea .
Wakazi wa eneo hilop wanasema kuwa walisikia milio ya
bunduki iliyodumu kwa dakika kadhaa .
Wanasema pia kuwa walisikia sauti za kelele za wanafunzi na
waalimu .
Wanajeshi wakijiandaa kwa makabiliano na wapiganaji wa
Taleban
Haijabainika wazi ni kwa namna gani wanamgambo wa Talebain
waliweza kupenya hadi kuingia ndani ya majengo hayo yanayomilikiwa na jeshi.
Jeshi la Pakistan limesema operesheni ya uokozi ilikuwa
ikiendelea na kwamba wengi wa wanafunzi na waalim wameokolewa toka eneo la
hatari.
Shambulio hilo limetokea wakati operesheni kubwa ya kijeshi
ikiendelea dhidi ya wapiganaji wa Taleban wa Pakistan na wanamgambo wengine
wanaoendesha harakati zao kaskazini mwa jimbo la Waziristan.chanzo Bbc
No comments:
Post a Comment