Nchini Tanzania, zoezi la kuboresha daftari la kudumu la
wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya unaojulikana kama Biometric Voter
Registration - BVR limekuwa likeendelea. BVR ni mfumo wa utambuzi wa wapigakura
wengi na kwa haraka kwa kutumia alama za kibailojia kama vidole, macho au
sauti.
Lengo la zoezi hili ni kuhakikisha utumiaji wa daftari hailo
jipya kwa ajili ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini
humo mwakani. Hivi karibuni makamu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Jaji
Mkuu mstaafu Zanzibar Hamid Mahamoud Hamid alikutana na viongozi wa vyama vya
siasa nchini kuwapa taarifa kuhusu kuanza kwa
shughuli za uboreshaji wa daftari
la kudumu la wapiga kura.
Tume imechukua hatua hiyo ili kuondokana au kupunguza utata
katika uchaguzi ambapo kwa mfumo wa kidigitali utadhibiti udanganyifu kwa
wapiga kura. Mpaka sasa tume ya taifa ya uchaguzi inaendelea kutoa mafunzo kwa
watendaji wa tume,ambao ndiyo watakuwa wakufunzi. Mashine ya BVR inauwezo wa
kuandikisha watu Zaidi ya 50 kwa saa.
No comments:
Post a Comment