Watu zaidi ya 8 wamenusurika kifo wakati wakiwa wamelala
nyumbani mwao mtaa wa heri manispaa ya
tabora, baada ya gari la mizigo aina ISUZU kuparamia nyumba yao, lilipomshinda
dereva alipokuwa akikata kona, ambapo mama mjazito aliyenusurika amekimbizwa
hospitalini akiwa na hali mbaya kutokan a na mshituko na hali yake ya ujauzito.
Wakizungumza na ITV wananchi na mashuhuda wa ajali hiyo
walioharibiwa thamani zao mbali mbali
wamesema kuwa, umefika wakati serikali
kubadili adhabu za madreva wazembe ambao wanaendesha vyombo vya usafiri bila
kuzingatia sheria zilizowekwa na serikali huku wakipoteza maisha ya wananchi na
mali zao.
Akizungumza na ITV
juu ya ajali hiyo na kubaini uzembe wa dereva wa gari hilo lenye namba za
usajili t 396 AGS, ambaye hakupatikana mara moja, kamanda wa polisi mkoani
tabora kamishina msaidizi Suzani Kaganda aliyefika eneo la ajali hiyo amesema
kuwa, mwendesha gari hilo atatafutwa na hatua
stahiki zitachukuliwa dhidi yake.
Aidha mmiliki wa nyumba hiyo bw.Ramadhani Musa Kaswezi,
anayeishi kijijini ilolangulu hakusema lolote akidai kikao cha familia kitatoa
maamuzi ili kuelezea hatua atakazochukua
kutokana na wapangaji wake wawili kubolewa nyumba.
CHANZO: ITV
No comments:
Post a Comment