Polisi wakabiliana na waandamajani waliovamia ofisi za
serikali Hong Kong
Wanaharakati wanaopigania demokrasia katika eneo la Hong
Kong, wamesababisha ofisi za serikali kufungwa asubuhi ya leo kufuatia usiku
wenye ghasia kwenye mitaa.
Maofisa 11 wa polisi walijeruhiwa na watu 40 kukamatwa huku
kampeni hiyo ikiingia mwezi wa tatu.
Serikali ya mji wa Hong Kong ililaani ghasia hizo ikisema
kuwa waandamanaji waliwarushia vifaa polisi.
Waandamanaji hao ambao wengi ni wanafunzi wanataka China
kuipa Hong Kong uhuru zaidi wa kumchagua kiongozi wao kwenye uchaguzi unaokuja.
Kadhalika waandamanaji hao, walikabiliana na polisi waliokuwa
wamejihami kwa virungu na malori ya maji wakiwarushia watu maji.
Jumatatu asubuhi amri ilitolewa ya kutimuliwa kwa
waandamanaji hao kutoka katika eneo walilokuwa wanafanyia maandamano yao.
Maandamano ya leo yamesababisha hofu ya ghasia au vurugu zaidi
kutokea miezi miwili tu baada ya maandamano mengine kutokea miezi miwili
iliyopita.
Waandamanaji hao wanasema wanataka wao kama watu wa Hong
Kong kuruhusiwa kuchagua viongozi wao katika uchaguzi wa mwaka 2017 bila ya
serikali ya China kuingilia kati.
China hata hivyo imesema itaruhusu wakazi wa Hong Kong
kuchagua viongozi wao lakini itawakagua wagombea wa nafasi ya waziri mkuu kabla
ya uchaguzi kufanyika.
Baada ya makabiliano ya Jumatatu asubuhi, kiongozi wa eneo
hilo, aliwaonya waandamanaji hao kutorejea katika eneo la maandamano.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment