WAGOMBEA wa nafasi za uenyekiti wa vitongoji 200 na wa
serikali za vijiji 17 katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, ambao ni wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa kutokana na vyama vingine vya siasa
kutokupata wagombea katika maeneo hayo.
Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi katika Wilaya ya Bunda,
Simoni Mayeye alimwambia mwandishi wa habari hizi jana kuwa wagombea 200 wa
vitongoji na wenyeviti 17 wa Serikali za Vijiji katika Wilaya ya
Bunda ambao ni
wa CCM wamepita bila kupingwa.
â€Å“Jumla ya wenyeviti wa vitongoji 200 na wa serikali za
vijiji 17 ambao ni wa CCM wamepita bila kupingwa, kwa sababu vyama vingine
havikuweka wagombea,†alisema.
Mayeye alisema kuwa katika Wilaya ya Bunda kuna jumla ya vijiji
701 na vitongoji 574 na kwamba katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Bunda, wenyeviti
wa vitongoji wawili wa CCM wamepita bila kupingwa, kikiwemo kitongoji cha
Manyamanyama na Balili Kilimani.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika nchini kote Desemba
14, mwaka huu, ambapo vyama mbalimbali vya siasa vitashiriki katika uchaguzi
huo.
Chanzo:Habari Leo
No comments:
Post a Comment