Pages

Monday, December 15, 2014

WAGOMBEA 200 WA CCM WAPITA BILA KUPINGWA

WAGOMBEA wa nafasi za uenyekiti wa vitongoji 200 na wa serikali za vijiji 17 katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, ambao ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa kutokana na vyama vingine vya siasa kutokupata wagombea katika maeneo hayo.
Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi katika Wilaya ya Bunda, Simoni Mayeye alimwambia mwandishi wa habari hizi jana kuwa wagombea 200 wa vitongoji na wenyeviti 17 wa Serikali za Vijiji katika Wilaya ya 


Bunda ambao ni wa CCM wamepita bila kupingwa.
“Jumla ya wenyeviti wa vitongoji 200 na wa serikali za vijiji 17 ambao ni wa CCM wamepita bila kupingwa, kwa sababu vyama vingine havikuweka wagombea,” alisema.
Mayeye alisema kuwa katika Wilaya ya Bunda kuna jumla ya vijiji 701 na vitongoji 574 na kwamba katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Bunda, wenyeviti wa vitongoji wawili wa CCM wamepita bila kupingwa, kikiwemo kitongoji cha Manyamanyama na Balili Kilimani.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika nchini kote Desemba 14, mwaka huu, ambapo vyama mbalimbali vya siasa vitashiriki katika uchaguzi huo.

 Chanzo:Habari Leo

No comments:

Post a Comment