Bill Gates anywa maji yaliotengezwa kutokana na kinyesi
Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amekunywa maji
yaliotengezwa kutokana na kinyesi cha binaadamu kama maonyesho ya teknologia
mpya itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea.
Mwanzilishi huyo wa Microsoft amesema kuwa ataisambaza
mitambo ya teknologia hiyo mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio
mwishoni mwa mwaka huu.
Teknologia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo
limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.
Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni
748 hawana maji safi ya kunywa.
katika kanda ya video iliowekwa katika blogi yake,Bwana Bill
Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya
kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.
''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote
yale niliokunywa,na baada ya kusomea teknologia hii nitayanya kila siku.
Maji haya ni salama kabisa'',aliandika katika blogi
yake.Kulingana na mtengenezaji wa mtambo huo Peter Janicki,maji taka hayo
huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo kutengwa na taka ngumu.
Taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke
unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakaazi
wa eneo hilo.
Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji
ili kutoa maji safi ya kunywa.
''lakini kwa nini mtu awe na wazo la kubadilisha uchafu kuwa
maji ya kunywa na umeme'',aliuliza Gates.
Jibu aliloandika ni kwamba kwa sababu magonjwa
yanayosababishwa na mazingira machafu huwaua watoto 700,000 kila mwaka na
huwakinga wengine wengi dhidi ya kuathirika kiakili na kimwili.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment