Magari ya kubebea abiria yaliochorwa Mombasa Kenya
Licha ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuruhusu magari
yanayobeba abiria nchini Kenya kuchorwa ama hata kupaka rangi yoyote ile,mabasi
mawili yaliochorwa picha yake yamekamatwa na maafisa wa polisi mjini Mombasa
Kenya.
Maafisa wa trafiki mjini Mombasa waliyakagua magari hayo na
kuyakamata magari yote yaliokuwa yamechorwa picha pamoja na magari yenye
madirisha yasioonyesha ndani.
Magari sita yakiwemo mawili yaliokuwa na picha ya Uhuru
yalikamatwa,licha ya agizo la rais kuruhusu wamiliki wa matatu kuchora picha
katika magari.
Uhuru alikuwa amesema kuwa hatua hiyo itawasaidia vijana
kutumia vipaji vyao ili kuweza kujinufaisha kimaisha.
Uchoraji katika magari hayo na muziki ulipigwa marufuku
mnamo mwaka 2003 na aliyekuwa waziri wa uchukuzi John Michuki.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment