Baada ya Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu iliyotumiwa
na polisi kwenye maandamano ya CUF jana tarehe 27 January ili ijadiliwe na
wabunge kama hoja ya dharura, spika Makinda aliamuru serikali ilete majibu
kesho ndio ijadiliwe.
Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda
aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya Serikali kuleta
majibu, hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta
kutoelewana kati ya wabunge
wa Upinzani na Spika. Ilibidi spika Anna Makinda kuahirisha bunge mpaka kesho
lakini baadae akabadili na kusema saa kumi jioni leo hii.
No comments:
Post a Comment