Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amepinga matamshi
ya Papa ya juma lilopita aliposema kuwa siyo sawa kufanya mzaha juu ya imani ya
watu wengine.
Akijibu kuhusu mashambulio yaliyofanywa na wapiganaji
Waislamu dhidi ya gazeti la Ufaransa la Charlie Hebdo, Papa alisema iwapo mtu
atamtusi mama ake, ataraji ngumi.
Bwana Cameron hata hivyo alisema katika nchi huru kuna haki
ya kukera kuhusu dini ya mtu mwengine.
Aliliambia shirika la habari la CBS la Marekani,
kwamba
vyombo vya habari vinafaa kuweza kuchapisha vitu ambavyo vinawakera baadhi ya
watu - ikiwa siyo kinyume na sheria.
No comments:
Post a Comment