Pages

Monday, January 19, 2015

CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI NYINGINE REAL MADRID IKISHINDA 3-0

 Cristiano Ronaldo ameandika historia nyingine katika  kitabu cha rekodi cha Real Madrid baada ya kufunga magoli mawili katika ushindi wa 3-0 waliovuna dhidi ya Getafe jioni kwenye mechi ya La Liga.
Hakuna mchezaji yoyote katika historia ya Real aliyefunga magoli mengi ya ugenini kumzidi Ronaldo ambaye amefunga mabao 27 na 28 katika msimu wa ligi.
Gareth Bale pia aliifungia Real Madrid dakika za lala salama, ingawa wakali hao wa Bernabeu walikwenda mapumziko bila kufunga goli.



No comments:

Post a Comment