Pages

Monday, January 19, 2015

MTOTO AMSHANGAZA RAIS MUSEVENI KWA KUONYESHA MAPENZI MAKUBWA KWAKE



 Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekutana na mtoto mdogo Boris Akanyijuka, aliyeonyesha kuwa ni shabiki yake mkubwa wakati akiwa ziarani katika hospitali ya rufaa ya Kabale.
 Mtoto Akanyijuka alisikika akiimba 'Museveni, Museveni' na kumkatiza mara kadhaa rais Museveni ambaye alikuwa akiongea. Mtoto huyo aliitwa ili kupewa mkono na rais, lakini kutokana na kumkubali mno rais alimkumbatia mguuni badala ya kumpa mkono.
Mtoto huyo alikaribishwa kukaa jukwaa kuu na akaenda moja kwa moja kukaa kiti cha rais na baadae alihamishiwa kiti kingine, ambapo baada ya mkutano rais Museveni alimpatia bahasha ya kaki ambayo haikujulikana ilikuwa na nini.

No comments:

Post a Comment