NYUMA ya ukaribu wa Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB),
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, kuna siri nzito kufuatia mambo mbalimbali
yanayojitokeza kati yao kila kukicha, Amani lina cha kukujuza.
Katika kuunga maelezo hayo, inasemekana kwamba mbali na
mambo mengine, hivi karibuni Diamond alimpelekea JK tuzo zake tano za kimataifa
alizotwaa mwaka 2014 kwa kuwa nyuma yake kulikuwa na sapoti kubwa ya mkuu huyo
wa nchi.
UKARIBU MKUBWAKwa mujibu wa chanzo cha karibu ambacho ni
‘mtu’ wa Diamond, staa huyo amekuwa ‘klozdi’ sana na JK kufuatia mambo yake
mengi ya msingi kuyafanya kwa kumshirikisha, kiasi kwamba kuna wakati Diamond
hata akikurupuka usiku wa manane kama ana jambo huwa hasiti kumpigia simu
mheshimiwa na kuongea kwa muda huku wakicheka weee!
IKULU
Habari hizo zilidai kwamba hata kama Diamond akishindwa
kuzungumza naye kwa simu, kukicha mguu na njia hadi ikulu na kuzama ndani kama
nyumbani kwao vile ambapo JK akiambiwa anasema ‘mwacheni aingie kijana wangu
atakuwa na shida huyo’.
‘Diamond Platnumz’ akibadilishana mawazo na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’. “Diamond amekuwa na
uhusiano wa karibu kwa kila jambo na JK kiasi kwamba hata yeye anamkubali
vilivyo hivyo huwa hasiti kumsapoti pale anapokuwa amekwama na hata kujivunia
ukaribu wake na Diamond kutokana na uchapakazi na nidhamu anayoionesha kwake
kadiri siku zinavyozidi kwenda.
“Huwezi ukaongea ishu ya muziki na JK asimtaje ‘mwanaye’
Diamond, ukaribu wao umepitiliza na inasemekana wana mikakati mikubwa ya
baadaye, ni siri nzito kwa kweli iliyopo baina yao na hakuna anayejua,”
kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Akizungumza na Amani kuhusu ishu hiyo, Diamond alimmwagia
sifa za kutosha JK huku akithubutu kuanika kwamba, haoni tena katika maisha
yake kama atakuja kutokea kiongozi wa juu wa nchi akawa na upendo wa hali ya
juu kwa wasanii wa Tanzania kama ilivyo kwa JK.
Tuzo ambazo Mkali ‘Diamond Platnumz’ alizifikisha kwa Rais
Jakaya Kikwete. “Kiukweli nampenda sana mheshimiwa (JK) na nimekuwa nikijiuliza
kila kukicha kama kweli nchi hii tutakuja kupata rais mwenye mapenzi ya dhati
na wasanii kama ilivyo sasa kwa baba yetu JK, maana ni mtu wa pekee sana kiasi
kwamba muda wowote kama una shida naye yuko wazi kuzungumza na kukupanua mawazo
tofauti na unavyoweza kufikiria.
KAMA MWANAFAMILIA
“Mara nyingi siku hizi ninapokutana na rais wetu nimekuwa
nikijisikia kama mwanafamilia kutokana na jinsi anavyoniongoza na kuthamini
kila kazi inayotokana na muziki wangu jambo ambalo ni la kujivunia sana kwenye
maisha yangu maana ninaona wasanii kibao katika nchi nyingine hawafanyiwi haya
tunayopata sisi wasanii wa Tanzania kutoka kwa mheshimiwa.“Nina uhuru mwingi
sana wa kuzungumza naye na amekuwa akifanya hivyo karibia kwa kila msanii na
kutambua hilo na ndiyo maana hata tuzo zangu nilizopata mwaka 2014 nilimjulisha
pamoja na yeye kujua na kunipongeza lakini pia mafanikio hayo naamini
yamepatikana kutokana na sapoti yake kubwa ambayo amekuwa akinipatia mara kwa
mara.
‘Diamond Platnumz’ akiwa katika pozi tofauti na rais wa
nchi. “Sidhani kama kweli tutakuja kupata rais wa aina hii ambaye amekuwa
akitambua kila shughuli na fani ya kila Mtanzania maana amekuwa akitujali sana
wasanii jambo ambalo halikuwahi kutokea hapo nyuma kwa marais waliopita,
husasan kwenye muziki wetu huu wa Bongo Fleva,” alisema Diamond.
MARA YA MWISHO KUKUTANA
Desemba 23, mwaka jana, Diamond alikutana na JK, ikulu
ambapo mbali na kumpongeza, walizungumza mambo mengi ikiwemo namna ya kujipanga
zaidi kimataifa huku akimweleza madhara ya umaarufu unaendana na kupata mkwanja
mrefu.
KUMBUKUMBU ZA HARAKA
Ndani ya makabrasha ya Amani, kumbukumbu zinaonesha kuwa,
Diamond ameshakutana na JK si chini ya mara kumi, nje ya nchi na ndani.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment