Akizungumza mchana huu katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu
wa Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha
malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa Tambwe
wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo wanataka
mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo likiwa ni kujua
umakini wa waamuzi hao.
“Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia
kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini
haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na Yanga
hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na hata Ruvu nao
tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao kushabikia maovu haya.
Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema
ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi
kuyaweka hadharani.
“Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni
jinsi gani unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa
wenzangu wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo
kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema Tambwe.CHANZO SHAFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment