Polisi nchini Ujerumani wanasema kuwa kumekuwa na shambuli
la kuchoma moto ofisi za gazeti ambalo lilichapisha vibonzo kutoka kwa gazeti
la vibonzo la Charlie Hebdo.
Mawe na vitu vinavyowaka moto vilirushwa katika dirisha la
ofisi za gazeti la Hambuger Morgenpost mapema leo Jumapili.
Vyumba viwili kwenye afisi hizo viliharibiwa lakini moto huo
ulizimwa kwa haraka na hakuna mtu aliyejeruwa.
Baadhi ya nakala zilizochomeka baada ya gazeti la Humbuger
Post kushambuliwa
Wiki iliyopita gazeti hilo lilichapisha picha za vibonzo vya
mtume Mohammed kutoka gazeti la ufaransa la Charlie Hebdo.
Makala kwenye tovuti ya gazeti hilo inasema
haijabainika
iwapo shambulizi hilo lina uhusiano na kuchapishwa kwa picha hizo.
Polisi mjni Hamburg wanasema kuwa wamewakamata vijana
kufuatia kisa hicho.
No comments:
Post a Comment