serikali ya Tanzania inatarajiwa kuingilia kati kuhusiana na
marafuku iliowekewa magari ya Utalii ya taifa hilo yanayosafirisha watalii kati
ya Arusha na Nairobi kutoingia katika uwanja wa Ndege wa JKIA jijini Nairobi.
Wahudumu wa magari hayo waligoma kwa masaa kadhaa wakingojea
msimamo wa serikali kuhusu marufuku hiyo iliowekewa magari hayo ya tanzania
mnamo mwezi Disemba mwaka jana.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, Waziri
wa mali asli na utalii Lazoro Nyalandu amewahakikishia wahudumu hao kwamba
atasafiri hadi jijini nairobi pamoja na wawakilishi wao ili kuzungumza kuhusu
swala hilo na mwenzake wa Kenya.
''Serikali yetu pia imeshangazwa na hatua hiyo ya
Kenya kwa
sababu viwanja vya ndege havihusiki katika makubaliano yalioafikiwa na mataifa
hayo jirani'',alisema.
Bwana Nyalandu amekiri kwamba Tanzania mwaka 1985
iliafikiana na kenya kupiga marufuku magari ya kenya ya Utalii kutoingia katika
mbunga zake za wanayama pori,hatua ambayo ililenga kuwawezesha wahudumu wa
magari ya Utalii ya nchini humo.
''Marufuku hiyo ya Kenya inamaanisha uwanja huo wa ndege
sasa ni kivutio cha watalii badala ya eneo la kuingilia Kenya'',alishangaa
Nyalandu akisema hatua hiyo imewagharimu wahudumu wa utalii nchini Tanzania.
Lakini wachanganuzi wanaamini kwamba marufuku hiyo ya Kenya
ni hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya hatua ya tanzania kufunga mpaka wa
Bolongoja uliopo kati ya mbuga ya wanayama pori ya Serengeti na masai Mara ya
Kenya miaka ya 70.chanzo bbc
No comments:
Post a Comment