Baloteli na Fanny walionekana kuwa pamoja kwa muda mrefu
kabla ya kuachana baada ya muda huku kukiwa hakuna sababu iliyowahi kutajwa na
yoyote kati ya wapenzi hao wa zamani ya kuachana kwao .
Balotelli alifikia hatua ya kumchumbia binti huyo raia wa
Ubelgiji mwenye asili ya Ethiopia akimvisha pete ya thamani ya paundi elfu
25,000 wakati wakiwa nchini Brazil .
Baloteli na Fanny wakati uhusiano wao ulipokuwa unaendelea .
Mwanadada huyo amefichua kuwa chanzo cha wawili hao kuachana
na kitendo cha Mario Baloteli kumlazimisha aachane na fani yake ya uanamitindo
pamoja na muziki .
Fanny amefichua kuwa Balotelli alikuwa hapendezewi na picha
za mitindo ambazo alikuwa akipiga , kimsingi hakuwa anakubaliana na kazi yake
hali iliyofanya arudishe pete yake ya uchumba na kusitisha mipango yao ya
kuoana.
Baloteli hakutaka Mpenzi wake Fanny Neguisha ajihusishe na
kazi ya urembo na mitindo pamoja na muziki .
Fanny alisema hayo kwenye mahojiano ya tele
visheni ambapo alisema kuwa Baloteli alimlazimisha aachane
na mitindo , ambapo mrembo huyo alisisitiza kuwa anaipenda kazi yake na ana
haki ya kuwa na maisha ya kazi kama ilivyo kwake (Balotelli) jambo ambalo Mario
hakukubaliana nalo
alotelli alimchumbia mrembo huyu mwaka jana nchini Brazil .
Fanny alirudisha pete ya Baloteli yenye thamani ya paundi
25,000 baada ya wawili hao kuachana .MAANDISHI NA Millard Ayo
No comments:
Post a Comment