Pages

Monday, January 19, 2015

Hofu mpya kwa watumiaji wa simu za mkononi


Unadhani simu yako ya mkononi ni kichaka kikubwa kinachoweza kuhifadhi siri zako zote?

Jibu ni hapana. Kwani teknolojia inamwezesha mtumiaji yeyote kuingilia mawasiliano katika simu yako na kufyonza taarifa mbalimbali  kama ujumbe mfupi, barua pepe, simu zinazotoka na kuingia, picha unazopiga au kutumiwa hata video, pia inaweza kubaini eneo alipo mtu.

 Kwa lugha nyepesi kitendo hiki huitwa udukuzi.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma anafafanua udukuzi akieleza kuwa ni matumizi ya teknolojia inayowezesha kuingilia mawasiliano ya mtu katika simu au kifaa chochote cha mawasiliano.


Udukuzi wa Serikali

Novemba mwaka jana, Kampuni ya Kimataifa ya Simu za Mkononi ya Vodafone, ilitoa taarifa 



inayoonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeweka nyaya za siri katika mtandao wa Vodacom  na kunasa mawasiliano ya wateja 98,765 kwa mwaka 2013.

Katika ripoti hiyo,(Law Disclosure Enforcement), Tanzania inatajwa kuwa ni nchi ya pili duniani miongoni mwa  nchi 29 ambazo Vodafone inatoa huduma ikiwa nyuma ya Italia kwa kufuatilia, kuingilia au kunasa mawasiliano ya simu.

Italia inashika nafasi ya kwanza kwa mawasiliano 605,601 ya raia wake kufuatiliwa na taasisi za kiusalama za Serikali.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba alidai kushtushwa na taarifa za Serikali kunak-ili mawasiliano ya simu kwa kutumia nyaya za siri.

 “Hata mimi imenishtua kidogo kwa sababu sheria za usalama za mawasiliano, kunakili chochote kunafanyika kwa sheria tu,” anasema.

Hata hivyo, Makamba anakiri kuwa Serikali kupitia taasisi za usalama hulazimika kuomba taarifa za wateja kwa ajili ya uchunguzi.
- Mwananchi

No comments:

Post a Comment