Katoto kachanga kalikotumbukizwa kwenye ndoo kwa zaidi ya
saa 3.No! Manesi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro wameingia kwenye kashfa nzito ya kusababisha kifo baada ya kudaiwa
kumtumbukiza mtoto mchanga kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3.
Tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo mkoani hapa lilijiri
hivi karibuni ambapo mwanamke aitwaye Zainabu lsmali, mkazi wa Kididimo jirani
na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine ‘SUA’ alishikwa na uchungu wa kujifungua
na kukimbizwa katika hospitali hiyo kwa msaada wa jirani yake aliyejitambulisha
kwa jina la Mama Sira Manga.
Ndoo iliyotumika. Akizungumza na Ijumaa Wikienda juu ya
tukio hilo, Mama Manga alikuwa na haya ya kusema: “Huu ni uzembe mkubwa wa
manesi. Tulipofika hospitali mtoto alizaliwa akiwa hai lakini alikuwa njiti
kwani alikaa tumboni kwa mama yake miezi 7 badala ya 9.
Ndugu wa mama akiwa na mtoto huyo. “Cha ajabu usiku huo
manesi baada ya kumcheki mtoto walisema ni wa kike lakini eti walidai amekufa
hivyo waliamua kuchukua matambara ya mzazi yaliyotumika kujifungua na kumzoa
mtoto huyo na kumuweka kwenye ndoo ambayo kwa kawaida sisi wazazi huwa
tunakwenda nazo leba.
“Walituambia tukazike, unajua kutoka hospitali hadi Kididimo
juu ya Milima ya Uluguru ni mbali na gari lilichelewa kutufuata hivyo mtoto
huyo alikaa kwenye ndoo zaidi ya saa 3.
Mama wa mtoto huyo, Zainabu lsmali “Tulipofika nyumbani na
kumtoa mtoto kwenye ndoo tukamuona anahema na kufumbua macho baada ya
kumtingisha akakohoa ndipo tukamkimbiza tena hospitali.Pamoja na jitihada za
manesi hao, kesho yake mtoto huyo alifariki dunia baada ya kitovu chake
kuingiza hewa kwani kilikuwa bado hakijakatwa.
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo. Mama wa mtoto huyo, Zainabu
alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema:
“Roho inauma sana lakini mzungumzaji wa tukio hilo ni mume
wangu.”
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo alipohojiwa na mwandishi wetu
alisema: “Ni kweli nimempoteza mwanangu lakini nisingependa kutoa lawama kwa
manesi kwani mke wangu bado anaendelea kuzaa.”
Mwandishi wetu alifika hospitalini hapo na kuzungumza na
daktari mfawidhi, Dokta Rita Lyamuya ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro,
Dokta Rita Lyamuya. “Ni kweli tukio hilo limetokea kwenye wodi yetu ya wazazi.
“Manesi walitimiza jukumu lao la kumhudumia mzazi lakini kwa
bahati mbaya tuna changamoto ya umeme kukatika bila taarifa hivyo wakati manesi
wakimzalisha alijifungua mtoto njiti.
“Ghafla umeme ulikatika na kutokana na giza, manesi walijua
mtoto amekufa hivyo waliwaeleza wanandugu kwamba mtoto amefariki dunia.
“Ndugu walimchukua walipofika kwao na kukitoa kwenye ndoo
walibaini mtoto bado yupo hai.
“Walimleta tena hapa hospitali na tulifanya juhudi za
kumtibu lakini kwa bahati mbaya amefariki dunia.”
No comments:
Post a Comment