Mambo ya fedha! Takribani wiki saba tangu anyakue zaidi ya
Sh. Milioni 500 baada ya kuibuka mshindi kwenye Shindano la Big Brother Africa
‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan anadaiwa kubakiza takribani kiasi cha Sh. milioni
200 baada ya kudaiwa kununua mjengo wa ghorofa wenye thamani ya zaidi ya Sh.
milioni 300.
Kwa mujibu wa Idris, nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi Beach
jijini Dar hivyo kwa sasa naye ni baba mwenye nyumba.
Mjengo wa ghorofa uliononuliwa na mshindi kwenye Shindano la
Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan.
Mjengo huo una vyumba kadhaa, sebule mbili, bustani na eneo
la kutosha la maegesho ya magari.
Habari zinadai kwamba kama kweli ametumia kiasi hicho cha
fedha huku akimshukuru mtu aliyemtaja kwa jina la Mohamed kwa kufanikisha jambo
hilo, basi atakuwa amebakizi milioni 200 ambazo wataalam wa mambo ya uchumi
wanamshauri kufungulia kampuni au biashara.
Idris Sultan akipozi mbele ya mali zake.
kulipia bili mbalimbali, kodi na kuajiri wahudumu.
“Anaweza akaona kwamba kununua nyumba ni matumizi mazuri ya
fedha alizoshinda lakini anatakiwa awe makini, aidha kwa kufanyia biashara au
kutoa huduma itakayokuwa ikimwingiza kipato.
“Pia asisikilize watu wanasema nini juu ya fedha zake.
Anatakiwa kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo kabla hajazipata,” alisema mmoja
wa wataalam hao ambaye hakupenda jina lake liandikwe.CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment