Hivi karibuni tumesikia watu wengi wakiwemo wasanii
wakilamika juu ya account zao pamoja na simu kuvamiwa na wezi wa mitandaoni,
watafiti wanasema matumizi ya password dhaifu pia huchangia account hizo
kuvamiwa, au wengine kutumia password moja kwenye account zaidi ya moja ikiwemo
email, simu na mitandao ya kijamii.
Utafiti uliofanywa na
kampuni ya SplashData, Marekani umeonyesha kuwa password milioni 3.3
zilizotumika mwaka 2014 katika maeneo ya Amerika ya Kaskazini na Ulaya
Magharibi zilivuja huku majina kama Michael, Thomas, Andrew na Daniel
yakionekana kuwa majina yanayotumiwa sana kwenye password.
Takwimu hiyo imeonyesha kuwa password nyingi
ambazo
zinatumika zimekuwa ni rahisi sana kiasi kwamba zinawapa urahisi hackers
kuzitabiria na kuweza kuvamia account hizo kirahisi na kushauriwa password
nzuri ni ya kuchanganya namba na tarakimu.
Utafiti huo umetoa password 25 zilizotumiwa na watu wengi
duniani kwa mwaka 2014, ambazo ni 2.2% ya password zote.
Hii ni list ya password hizo 25 ambazo zimetumika zaidi 2014.
:: 123456
:: password
:: 12345
:: 12345678
:: qwerty
:: 1234567890
:: baseball
:: dragon
:: football
:: 1234567
:: monkey
:: letmein
:: abc123
:: 111111
:: mustang
:: access
:: shadow
:: master
:: michael
:: superman
:: 696969
:: 123123
:: batman
:: trustno1
No comments:
Post a Comment