Mwanasayansi wa zamani katika mahabara ya kitaifa mjini Los
Amos nchini Marekani amefungwa jela miaka mitano kwa kujaribu kuipatia nchi ya
Venezuela siri za kutengeza bomu la nuklia.
Pedro Leonardo Mascheroni alikiri kosa mwaka 2013 la kutoa
siri kwa jasusi wa FBI aliyejidai kuwa afisa mkuu kutoka Venezuela.Pedro Mascheroni, mwenye umri wa miaka 79,anatoka nchini
Argentina.Mkewe pia alifungwa jela mwaka mmoja.Mascheroni alikuwa anachunguzwa kwa karibu mwaka mmoja kabla
ya kuchukuliwa hatua.Shirika la ujasusi la FBI, lilinasa komputa, barua , picha
na vitabu kutoka nyumbani kwa mwanasayansi huyo.Kulingana na stakabadhi za mahakamani, bwana Mascheroni
aliambia afisaa huyo wa FBI kwamba angeweza kuisiadia Venezula kutengeza bomu
la nuklia kwa kipindi cha miaka kumi.
Alisema nchi hio ingeweza kutengeza mtambo wa kisiri wa
nuklia chini ya ardhi kuisiaidia kurutubisha madini ya Plutonium.Aliongeza kwamba pia
angeisaidia Venezuela kuzalisha kawi ya
nuklia
Bwana Mascheroni alifanya kazi kwa karibu miaka kumi katika
kitengo cha kutengeza zana za nuklia katika mahabara ya kitaifa ya Marekani
ambako bomu la kwanza la Atomiki lilitengezwa.
Mkewe alikuwa mwandishi wa maswala ya teknolojia katika
mahabara hio.
Aliachishwa kazi mwaka 1988
Katika mahojiano na shirika la habari la AP, alisema
alifanya mawasiliano na nchi nyingine baada ya wazo lake la kutengeza kawi safi
ya nuklia kukataliwa na maafisa wa baraza la Congress.
Mascheroni alisema alifanya mazungumzo na Venezuela, baada
ya Marekani kukata wazo lake la kuzalisha kawi safi ya nuklia.
Serikali ya Marekani,imesema kuwa haiamini kuwa Venezuela
ilikuwa inajaribu kuiba siri zake za kutengeza zana za nuklia.
No comments:
Post a Comment