Rais Salva Kiir
Mkutano wa viongozi wa kikanda ulioandaliwa kujadili mgogoro
wa mwaka mmoja unaotokota nchini Sudan Kusini, umecheleweshwa baada ya Rais
Salva Kiir kuugua na kukimbizwa hospitalini mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Afisa mmoja wa shirika la IGAD, ambalo linafanya juhudi za
kuwakutanisha viongozi wa Sudan Kusini kwa lengo la kumaliza vita, aliambia BBC
kwamba Rais Kiir, alianza kuvuja damu kutoka puani
Kabla ya kuugua, hapo jana Kiir alifanya mazungumzo na
kiongozi wa waasi Riek Machar ambapo alimtaka kupuuzilia mbali maswala
yanayochochea mgogoro huo ili kumaliza mgogoro huo ambao umedumu mwaka mmmoja
Viongozi wa kikanda, wanakutana baadaye leo, kushinikiza
pande zote kufikia makubaliano ili kumaliza vita.
Swala kuu kwenye ajenda, ni kusuluhisha maswala yanayoleta
kizungumkuti kuhusu serikali ya muungano kama moja ya suluhu la kupatikana
amani.
Pande zote zinazozozana zimekosa kufikia makubaliano kuhusu
wadhifa wa waziri mkuu na ikiwa anapaswa kuwa na mamlaka makuu au la.
Maelfu ya watu wamefariki na wengine zaidi ya milioni moja
kuachwa bila makao tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka nchini humo
Disemba mwaka 2013.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment