Manchester City wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa
Swansea Wilfried Bony kwa pauni milioni 28.
Bony, 26, ameingia mkataba wa miaka minne na nusu kwenda
Etihad na atavaa jezi namba 14.
"Ni furaha kubwa kwangu, na heshima kubwa kuwa hapa, ni
changamoto nzuri." amesema. Bony alijiunga na Swansea kwa pauni milioni 12
akitokea Vitese Arnhem mwaka 2013 na alikuwa mfungaji bora wa mwaka wa kalenda
2014 akipachika mabao
20 katika EPL. Klabu hAzo mbili zilifikia makubaliano
mwisho wa wiki, ambapo pauni milioni 25 zimelipwa taslimu, huku zilizosalia
milioni 3 zitatolewa kulingana na jinsi atakavyoonesha kiwango. Uhamisho huo
unafunika uhamisho wa Yaya Toure wa pauni milioni 24 mwaka 2010, na hivyo
kumfanya Bony kuwa mchezaji wa gharama zaidi katika historia, kutoka Afrika.
No comments:
Post a Comment