Lakini kuna kitu ambacho hakukitegemea kilichokuwa
kinamuandama kufuatia uwezo wake michezoni alipokuwa Equatorial Guinea mwaka
2008 katika michuano ya soka la wanawake wa mataifa ya Afrika.
Goli lake la ushindi katika ardhi ya nyumbani,na timu yake
kuwa ya kwanza wakiifuatia Nigeria ,ambayo iliibuka kuwa washindi wa
jumla,Anonma badala ya kuhesabika kuwa mkombozi na mwenye kuitimiza ndoto yake
michezoni, badala yake amebaki njia panda.
Anonma awapo uwanjani huwa ana haha uwanjani huku na kule na
nguvu alo nayo,timu pinzani humbeza kuwa hawezi kuwa mwanamke bali wanacheza na
janadume,na ndipo sasa kituko kikaja kutokana na tuhuma hizo shirikisho la soka
barani Africa walichagua njia ya kuhakiki jinsia ya Anonma.
Genoveva Anonma mwanasoka mwenye jinsi ya kike mwenye kasi
ya ajabu michezoni aliamriwa kuvua nguo zake zote mbele ya maafisa wa CAF na mbele
ya timu yake ya Equatoria Guine,nilifedheheka mno,hata ari ya mchezo ilishuka
na nilikuwa nalia mno,ilikuwa ni udhalilishaji tosha,lakini ilinilazimu
kutekeleza amri.
MAISHA YAKE.
Genoveva Anonma amekulia Equatorial Guinea na kadiri joto la
kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika upande wa wanaume ikitarajiwa
kuanza mwishoni mwa juma,tamaa yake ya kuwa
msukuma gozi uwanjani inazidi
kupanda,na tamaa hii haikuanza leo bali alipokuwa shuleni na hata nyumbani pia.
Anonma ameichezea Turbine Potsdam nchini Ujerumani katika
ligi maarufu ya Bundesliga tangu mwaka 2011 .
Naye anasema,nilipokuwa na miaka mitano,huko kijijini kwetu
wasichana walikuwa hawataki kucheza na mimi kwasababu nilikuwa napenda kucheza
mpira wa miguu tu,hivyo muda mwingi nilikuwa nikicheza na wavulana tu anasema
Anonma.
Baba yangu alikuwa anaishi katika mji mwingine na mwanamke
mwingine, na mama yangu alikuwa akipambana name kila wakati niache kucheza
mpira wa miguu,alikuwa akinitaka nisome hadi kufikia hatua ya digirii na niwe
mwalimu ama nibobee katika masuala ya kuwasaidia watoto.
Tulikuwa hatuelewani,na akaapa kuwa hataki kuniona tena,name
nikaondoka nyumbani na kwenda kuishi na mjomba wangu,mjombaangu hakuwa na
matatizo nami akanipeleka mjini huko nikaendelea na masomo yangu na sikuacha
kucheza mpira .
Anonma akapewa nafasi katika mji mkuu wa nchi yake Malabo
alipokuwa na umri wa miaka 15 nazungumzia mwaka 2002.Hakuishia hapo mwaka mmoja
baadaye alijiunga na timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini,na baadaye
akajiunga Jena ya Ujerumani ilikuwa katika ligi ya Bundesliga akiwa na timu
hiyo aliwika na kuwa mfungaji bora wa Jena kwa misimu miwili mfululizo.
Mshindi wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka
2011 Nigeria, pamoja nan chi zingine ikiwemo Afrika Kusini,Ghana, waliishutumu
Guinea kwakuwa na wachezaji watatu wa kiume katika timu yao wachezaji hao ni
ndugu wawili Salimata na Bilguisa Simpore, na nahodha wao Anonma.
Taarifa za watatu hao kuwa ni wanaume zilipoanza kusambaa
katika mitandao ya kijamii Anonma akaamua kuvunja ukimya na kwenda mbele ya
vyombo vya habari kukana shutuma hizo.
Na Anonma anadai kuwa yote hayo yanakuja kwasababu yey ni
mwepesi na mwenye kasi ya ajabu awapo mchezoni,lakini najitambua kuwa mimi ni
mwanamke.
No comments:
Post a Comment