Stori: Musa mateja/Risasi
STAA aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa
Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’ ameibuka na kumvaa mwanadada Judith
Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’ akidai amemdhalilisha kwa mashabiki wake.
Staa aliyewahi kukamata vilivyo kwenye anga ya muziki wa
Bongo Fleva, Shabani Ramadhani ‘Matonya’
Akizungumza na mwanahabari wetu, Matonya alisema anamtafuta
Jide popote alipo ili amuulize kinaga ubaga kwa nini aliamua kuposti picha
kwenye mitandao yake ya kijamii ikimuonesha akiwa hajitambui pasipo kumtaarifu.
Mwanadada Judith Wambura ‘Jide au Lady Jaydee’.
“Nimeumizwa sana na Jide kwa kitendo chake cha kuamua
kunidhalilisha kwa kiasi hicho tena akijua mimi ni mwanamuziki mwenzake na kama
kuna kitu aliona simfurahishi kwenye mwenendo wa maisha yangu basi alikuwa wazi
kuniita na kunikalisha chini na siyo kama uamuzi alioutumia wa kunianika kwenye
mitandao,” alisema Matonya.
Matonya alifafanua kuwa picha hiyo alipigwa katika video
yake mpya lakini Jide akaichukua na kuiweka mitandaoni pasipo kumuuliza.
Matonya akiwa mtungi.
“Ile picha aliyoitumia kunidhalilisha ilikuwa ni ya video
yangu ya wimbo mpya unaoitwa Homa ya Jiji ambayo itatoka hivi karibuni, sasa
yeye ameweka mitandaoni na kusababisha watu wanidharau kwa kuona nimelewa
chakari, asiponiomba radhi nitahakikisha namfikisha mahakamani,” alisema
Matonya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jide aliiposti picha ya
Matonya akiwa amelala na kusindikiza na ujumbe ulioonesha kama hamjui msanii
huyo hali iliyosababisha mashabiki wengi kumsema vibaya Matonya.
No comments:
Post a Comment