Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti
_______________________
_______________________
Na demasho.com
Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
imefanya tahimini ya elimu ya na matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi
mwaka 2014 katika ukumbi wa EMAU Peremiho.
Katika tathimini hiyo mkuu wawilaya ya Songea
Joseph Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa, Watendaji wa kata na Watendaji wa Vijiji kuwapa elimu wazazi
juu ya umuhimu wa kuchangia chakula cha kutosheleza muhula wa masomo
ili kusaidia wanafunzi kufanya vizuri katika masomo
“
Kwani kufanya hivo kutasaidia
wanafunzi kujifunza muda wote wawapo shuleni na kujenga ushirikiano baina yao
wanapokuwa pamoja na hali hiyo iatainua kiwango cha ufaulu” alisema Mkirikiti.
Hata hivyo Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa,
Watendaji wa kata na Watendaji kuacha
kusingizia wanasiasa kuwa wamezuia suala la kuchangia chakula
“
Tabia ya kuwasingizia
wanasiasa kuwa wamezua kuchangia chakula mashuleni muache sio kila kitu
kusingizia wanasiasa hivi ni kiongozi gani asiependa maendereo ?, maana saiz
kila kitu wanasiasa wamezuia hasa kipindi hiki tunachoenda cha uchaguzi
utasikia wanasiasa wamezuia ukiona mwanasiasa anazuia basi huyo ni SHIDAAA ”Alisema Mkirikiti.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Songea vijijini - Sigsibert Valentine akitoa hoja katika tathimini ya elimu kwa Halmashauri yake ya Songea Vijini.
--------------------
Naye Kaimu Afisa elimu wilya Bw. Tanu Kameka
ameomba baada ya Tathimini hiyo wakutane na waratibu wakata, wazazi , walimu
pamoja na watendaje ili uongezwe muda wa ziada wa ufundishaji ili kuweza kuleta
mwamko wa elimu katika halmashauri hiyo ya Songea vijijini na kuleta ufaulu
mzuri.
“ Miaka yote tumekuwa tukifanya hivo na ndiyo maana
tukawa tunaongoza katika matokeo , ila kwa mwaka jana hatukuweza kusimamia hili
swala la muda wa ziada ndiyo maana tumeshuka ila kwa mwaka huu tunalirudisha
swala la muda wa ziada hivyo tutafanya vizuri katika matokeo” Alisema Bw.
Kameka.
Madiwani ,Maafisa tarafa, Watendaji wa kata wakifatilia kwa makini maazimio yanayotolewa ili kuinua elimu katika halmashauri ya Songea Vijijini.
------------------
Halmashauri ya Wilaya
ya Songea Vijijini ina jumla ya shule 91,Katika matokeo ya mwaka jana
yaliyotoka mwaka huu mwanafunzi SHAFII ISSA wa shule ya Msingi PERAMIHO amekuwa
wa kwanza kiwilaya kwa wavulana kwa kupata wastani wa ufaulu alama 219 na
msichana HOPE NDUNGURU wa shule ya msingi CHIPOLE amekuwa wa kwanza kiwilaya
kwa kupata wastani wa ufauru wa alama 208.
No comments:
Post a Comment