faransa imegubikwa na hofu baada ya mashambulizi ya Januari
8 dhidi ya jarida la Charlie Hebdo
Mtoto mwenye umri wa miaka 8 alihojiwa na polisi nchini
Ufaransa kwa nusu saa Jumatano baada ya madai kwamba alitoa matamshi ya
kuwasifu magaidi akiwa shuleni.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la AP, mtoto huyo
alikataa kuungana na wenzake darasani kwa kimya cha dakika moja kuwakumbuka
watu 12 waliouawa na wanaume wawili waliokuwa wamejihami mjini Paris Ufaransa
mapema mwezi huu.
Shambulizi lilitokea katika ofisi za jarida la vibonzo la
Charlie Hebdo Januari tarehe saba kufuatia hatua ya jarida hilo kuchapisha
picha za kumkejeli mtume Mohammad wa dini ya kiisilamu.
Wahariri wakuu wa jarida hilo pamoja na wafanyakazi wenginge
waliuawa.
Mwalimu wa mtoto huyo alisema kuwa hakukataa tu kuungana na
wenzake kwa kimya cha dakika moja bali pia aliwasifu washambuluaji.
Na kwa sababu ya hali ya usalama ilivyo nchini Ufaransa kwa
sasa, mwalimu mkuu aliamua kumripoti mtoto huyo kwa polisi. Hata hivyo afisaa
mmoja alisisitiza kwamba hakuna malalamiko yaliwasilishwa dhidi ya mtoto huyo.
"tulimwita mtoto huyo na babake kujaribu kuelewa ni
vipi mtoto mwenye umri wa miaka 8 ana mawazo ya itikadi kali hivyo,'' alisema
Marcel Authier afisaa mkuu wa mawasiliano katika eneo hilo.
"bila shaka mtoto huyu haelewi anachosema lakini ni
muhimu kwetu kuhoji mawazo kama haya'' alisema Marcel.
Wakili wa mtoto huyo, Sefen Guez Guez, hakuweza kupatikana
kwa maoni yake lakini kwenye akauti yake ya Tiwtter alisema kuwa mtoto huyo
alikiri kusema: ''Ninawaunga mkono magaidi''.
Wakati polisi walipomhoji maana ya ''ugaidi'' mtoto huyo
alisema '' sijui''
" Baba huyo na mtoto wake walishangazwa na namna
walivyohojiwa, hali inayoonyesha wazi wasiwasi ambao umekumba Ufaransa tangu
mashambulizi yaliyofanywa mapema mwezi huu'' ilisema taarifa ya shirika
linalopambana na hofu dhidi ya waisilamu.chanzo BBC
No comments:
Post a Comment